Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 109 - يُوسُف - Page - Juz 13
﴿وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰٓۗ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۗ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ ﴾
[يُوسُف: 109]
﴿وما أرسلنا من قبلك إلا رجالا نوحي إليهم من أهل القرى أفلم﴾ [يُوسُف: 109]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hatukuwatuma kabla yako, ewe Mtume, kwa watu isipokuwa wanaume miongoni mwao ambao tunawateremshia wahyi wetu, na wao ni miongoni mwa watu wa mijini, kwani hao wana uwezo zaidi wa kuuelewa ulinganizi na ujumbe, wawaamini wenye kuongoka kwenye haki na wawakanusha wenye kupotea njia yake. Basi si watembee katika ardhi wajionee ulikuwa vipi mwisho wa wakanushaji waliopita na ni maangamivu gani yaliyowashukia? Na malipo mema ya Nyumba ya Akhera ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani, kwa walioamini na wakamuogopa Mola wao. Basi hamfikirii mkazingatia |