Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 31 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿فَلَمَّا سَمِعَتۡ بِمَكۡرِهِنَّ أَرۡسَلَتۡ إِلَيۡهِنَّ وَأَعۡتَدَتۡ لَهُنَّ مُتَّكَـٔٗا وَءَاتَتۡ كُلَّ وَٰحِدَةٖ مِّنۡهُنَّ سِكِّينٗا وَقَالَتِ ٱخۡرُجۡ عَلَيۡهِنَّۖ فَلَمَّا رَأَيۡنَهُۥٓ أَكۡبَرۡنَهُۥ وَقَطَّعۡنَ أَيۡدِيَهُنَّ وَقُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا هَٰذَا بَشَرًا إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا مَلَكٞ كَرِيمٞ ﴾
[يُوسُف: 31]
﴿فلما سمعت بمكرهن أرسلت إليهن وأعتدت لهن متكأ وآتت كل واحدة منهن﴾ [يُوسُف: 31]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Aliposikia mke wa Kiongozi kusengenya kwao na hila zao za kumtukana yeye, aliwatumia ujumbe na kuwaita kuja kumtembelea, na akatayarisha mito ya kutegemea na chakula cha kula, na akampa kila mmoja miongoni mwao kisu cha kukatia chakula kisha akasema kumwambia Yūsuf, «Jitokeze kwao.» Walipomshuhudia, walimuona ni kitu kikubwa chenye haiba, na wakashikwa na babaiko la uzuri wake na kuvutia kwake, wakajikata mikono yao katika hali ya kukata chakula kwa babaiko kuu na mshangao, na wakasema kwa kustaajabu, «Twajilinda na Mwenyezi Mungu! Huyu si binadamu!» kwa kuwa uzuri wake sio ule ujulikanao kwa wanadamu, «Huyu si mwingine isipokuwa ni mtukufu miongoni mwa Malaika.» |