Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 65 - يُوسُف - Page - Juz 13
﴿وَلَمَّا فَتَحُواْ مَتَٰعَهُمۡ وَجَدُواْ بِضَٰعَتَهُمۡ رُدَّتۡ إِلَيۡهِمۡۖ قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مَا نَبۡغِيۖ هَٰذِهِۦ بِضَٰعَتُنَا رُدَّتۡ إِلَيۡنَاۖ وَنَمِيرُ أَهۡلَنَا وَنَحۡفَظُ أَخَانَا وَنَزۡدَادُ كَيۡلَ بَعِيرٖۖ ذَٰلِكَ كَيۡلٞ يَسِيرٞ ﴾
[يُوسُف: 65]
﴿ولما فتحوا متاعهم وجدوا بضاعتهم ردت إليهم قالوا ياأبانا ما نبغي هذه﴾ [يُوسُف: 65]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na walipofungua vyombo vyao walipata kwamaba thamani ya bidhaa waliyoitoa wamerudishiwa. Wakasema, «Ewe baba yetu! Tuombe nini zaidi ya hii? Hii ni thamani ya bidhaa zetu, Kiongozi ameturudishia, basi kuwa na utulivu kuhusu ndugu yetu na muache aende na sisi ili tupate kuwaletea watu wetu chakula kingi, tumtunze ndugu yetu na tupate kuongeza twesha ya ngamia kwa ajili yake. Kwani Kiongozi anampimia kila mtu twesha ya ngamia mmoja; na hilo ni jambo jepesi kwake.» |