Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 112 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا قَرۡيَةٗ كَانَتۡ ءَامِنَةٗ مُّطۡمَئِنَّةٗ يَأۡتِيهَا رِزۡقُهَا رَغَدٗا مِّن كُلِّ مَكَانٖ فَكَفَرَتۡ بِأَنۡعُمِ ٱللَّهِ فَأَذَٰقَهَا ٱللَّهُ لِبَاسَ ٱلۡجُوعِ وَٱلۡخَوۡفِ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ ﴾
[النَّحل: 112]
﴿وضرب الله مثلا قرية كانت آمنة مطمئنة يأتيها رزقها رغدا من كل﴾ [النَّحل: 112]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu Amepiga mfano wa mji wa Makkh. Ulikuwa uko kwenye salama ya kutofanyiwa uadui, utulivu kutokana na dhiki za maisha na unajiliwa na riziki zake kwa uzuri na usahali kutoka kila upande, wakazi wake wakazikanusha neema za Mwenyezi Mungu kwao, wakamshirikisha na wasimshukuru, hapo Mwenyezi Mungu Akawatesa kwa njaa na kicho kwa kuviogopa vikosi vya Mtume, reheme ya Mwenyezi Mungu na amni zimshukiye, na majeshi yake yaliyokuwa yakiwatisha, na hili ni kwa sababu ya ukafiri wao na vitendo vyao vya ubatilifu |