Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 124 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿إِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبۡتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ ﴾
[النَّحل: 124]
﴿إنما جعل السبت على الذين اختلفوا فيه وإن ربك ليحكم بينهم يوم﴾ [النَّحل: 124]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ameufanya utukuzaji wa siku ya Jumamosi, kwa kuitenga kwa kufanya ibada ndani yake, kwa Myahudi ambao walitafautiana na Nabii wao juu yake, na wakaiteua badala ya siku ya Ijumaa ambayo waliamrishwa waitukuze. Hakika Mola wako , ewe Mtume, ni Mwenye kuhukumu baina ya wale waliotafautiana na Nabii wao Siku ya Kiyama na kumlipa kila mmoja kwa yale anayofaa kuyapata |