Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 125 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿ٱدۡعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلۡحِكۡمَةِ وَٱلۡمَوۡعِظَةِ ٱلۡحَسَنَةِۖ وَجَٰدِلۡهُم بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ ﴾
[النَّحل: 125]
﴿ادع إلى سبيل ربك بالحكمة والموعظة الحسنة وجادلهم بالتي هي أحسن إن﴾ [النَّحل: 125]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Lingania, ewe Mtume, wewe na aliyekufuata, kwenye Dini ya Mola wako na njia Yake iliyolingana sawa kwa kutumia hekima ambayo Mwenyezi Mungu alikuletea wahyi nayo ndani ya ya Qur’ani na Sunnah. Na uwazungumzie watu kwa njia inayolingana na wao, uwape nasaha kwa njia nzuri yenye kuwavutia kwenye kheri na kuwakimbiza wajiepushe na shari, na ujadiliane na wao kwa njia nzuri za kujadiliana za utaratibu na upole, kwani si juu yako isipokuwa ni kufikisha ujumbe, na ushafikisha. Ama kuwafanya waongoke, hilo ni juu ya Mwenyezi Mungu Peke Yake. Yeye Ndiye Anayemjua zaidi yule aliyepotea na akaiyepuka njia Yake, na Yeye Anawajua zaidi walioongoka |