×

SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka 17:1 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Isra’ ⮕ (17:1) ayat 1 in Swahili

17:1 Surah Al-Isra’ ayat 1 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 1 - الإسرَاء - Page - Juz 15

﴿سُبۡحَٰنَ ٱلَّذِيٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلٗا مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِي بَٰرَكۡنَا حَوۡلَهُۥ لِنُرِيَهُۥ مِنۡ ءَايَٰتِنَآۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ ﴾
[الإسرَاء: 1]

SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona

❮ Previous Next ❯

ترجمة: سبحان الذي أسرى بعبده ليلا من المسجد الحرام إلى المسجد الأقصى الذي, باللغة السواحيلية

﴿سبحان الذي أسرى بعبده ليلا من المسجد الحرام إلى المسجد الأقصى الذي﴾ [الإسرَاء: 1]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Anajisifu na kujitukuza kwa uweza Wake juu ya yasiyowezekana na yoyote isipokuwa Yeye, hapana Mola isipokuwa Yeye, hapana Mlezi isipokuwa Yeye. Yeye Ndiye ambaye Aliyempeleka mja Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kipindi cha usiku, kwa mwili wake na roho yake, katika hali ya kuangaza na siyo ya kulala, kutoka msikiti wa Ḥarām Uliyoko Makkah, kwenda msikiti wa Aqṣā uliyoko Bayt al- Maqdis, ambao Mwenyezi Mungu Amezibariki sehemu zinazouzunguka kwa matunda, nafaka na vinginevyo, na Akaufanya ni mahali pa Manabii wengi, ili ajionee maajabu ya uweza wa Mwenyezi Mungu na dalili za upweke Wake. Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kutukuka, Ndiye Mwenye kuzisikia sauti zote, Ndiye Mwenye kukiona kila cha kuonekana, na Atampa kila mmoja anachofaa kupata duniani na Akhera
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek