×

Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, 18:29 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Kahf ⮕ (18:29) ayat 29 in Swahili

18:29 Surah Al-Kahf ayat 29 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 29 - الكَهف - Page - Juz 15

﴿وَقُلِ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكُمۡۖ فَمَن شَآءَ فَلۡيُؤۡمِن وَمَن شَآءَ فَلۡيَكۡفُرۡۚ إِنَّآ أَعۡتَدۡنَا لِلظَّٰلِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمۡ سُرَادِقُهَاۚ وَإِن يَسۡتَغِيثُواْ يُغَاثُواْ بِمَآءٖ كَٱلۡمُهۡلِ يَشۡوِي ٱلۡوُجُوهَۚ بِئۡسَ ٱلشَّرَابُ وَسَآءَتۡ مُرۡتَفَقًا ﴾
[الكَهف: 29]

Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae. Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu Moto ambao utawazunguka kama khema. Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka. Yatayo wababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وقل الحق من ربكم فمن شاء فليؤمن ومن شاء فليكفر إنا أعتدنا, باللغة السواحيلية

﴿وقل الحق من ربكم فمن شاء فليؤمن ومن شاء فليكفر إنا أعتدنا﴾ [الكَهف: 29]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na usme kuwaambia hawa walioghafilika, «Haya niliyowaletea ndio ukweli utokao kwa Mola wenu. Basi yoyote kati yenu atakye kuamini na akafanya matendo yanayolingana na hiyo Imani, na afanye kwani hilo ni bora kwake, na mwenye kutaka kukanusha na akanushe kwani atakua hakumdhulumu yoyote isipokuwa nafsi yake mwenyewe. Hakika sisi tumewatayarishia makafiri Moto mkali ambao kuta lake limwazunguka. Na makafiri hawa wakitaka msaada Motoni wapatiwe maji kwa vile kiu ilivyo kali, wataletewa maji kama mafuta machafu yaliyo moto sana yanayochoma nyuso zao. Ni kibaya kilioje kinywaji hiki ambacho hakiondoi kiu yao bali kinaizidisha na ni ubaya ulioje wa Moto kuwa ndio mashukio yao na makazi. Katika haya pana onyo na tishio kali kwa yoyote mwenye kuipa mgongo haki na asiuamini utume wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na asifanye vitendo vinavyolingana na Imani hiyo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek