Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 56 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿وَمَا نُرۡسِلُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَۚ وَيُجَٰدِلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِٱلۡبَٰطِلِ لِيُدۡحِضُواْ بِهِ ٱلۡحَقَّۖ وَٱتَّخَذُوٓاْ ءَايَٰتِي وَمَآ أُنذِرُواْ هُزُوٗا ﴾
[الكَهف: 56]
﴿وما نرسل المرسلين إلا مبشرين ومنذرين ويجادل الذين كفروا بالباطل ليدحضوا به﴾ [الكَهف: 56]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hatuwatumilizi Mitume kwa watu isipokuwa wawe ni wenye kuwabashiria Pepo wenye Imani na matendo mema na kuwatisha na Moto wenye kukanusha na kuasi. Na pamoja ya kuwa haki ifunushie wazi, wale waliokanusha wanagombana na mitume wao kiubatili kwa njia ya upotufu, ili wapate kuiondoa, kwa ubatilifu wao, haki aliyokuja nayo Mtume, na wamekifanya kitabu changu, hoja zangu na adhabu ambayo walionywa nayo kuwa ni shere na ni kitu cha kufanyiwa mzaha |