Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 86 - الكَهف - Page - Juz 16
﴿حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَغۡرِبَ ٱلشَّمۡسِ وَجَدَهَا تَغۡرُبُ فِي عَيۡنٍ حَمِئَةٖ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوۡمٗاۖ قُلۡنَا يَٰذَا ٱلۡقَرۡنَيۡنِ إِمَّآ أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّآ أَن تَتَّخِذَ فِيهِمۡ حُسۡنٗا ﴾
[الكَهف: 86]
﴿حتى إذا بلغ مغرب الشمس وجدها تغرب في عين حمئة ووجد عندها﴾ [الكَهف: 86]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mpaka alipofika Dhulqarnain upande wa jua la kuchwa, alilikuta jua kwa vile alivyoliona kama kwamba linakuchwa ndani ya chemchemu ya maji moto yenye udongo mweusi, na akawakuta watu upande huo wa jua la kuchwa. Tulisema, «Ewe Dhulqarnain! Ima uwaadhibu kwa kuwaua au kwa linginelo, iwapo hawatakubali upweke wa Mwenyezi Mungu au uwatendee wema uwafundishe uongofu na uwaonyeshe usawa.» |