Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 175 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلضَّلَٰلَةَ بِٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡعَذَابَ بِٱلۡمَغۡفِرَةِۚ فَمَآ أَصۡبَرَهُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ ﴾
[البَقَرَة: 175]
﴿أولئك الذين اشتروا الضلالة بالهدى والعذاب بالمغفرة فما أصبرهم على النار﴾ [البَقَرَة: 175]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hao wanaosifika na sifa hizi wamechagua upotevu wakaacha uongofu, na wakachagua adhabu ya Mwenyezi Mungu wakaacha msamaha wake. Ni ujasiri ulioje wao wa kuchagua Moto kwa kufanya vitendo vya watu wa Motoni! Anastaajabu Mwenyezi Mungu kwa kujitokeza kwao kulifanya hilo. Basi oneni ajabu, enyi watu, juu ya ujasiri wao na uvumilivu wao kwenye Moto na kukaa kwao humo. Maneno haya yametumika kwa njia ya kuwatweza na kuwachezea |