×

Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, 2:187 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:187) ayat 187 in Swahili

2:187 Surah Al-Baqarah ayat 187 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 187 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿أُحِلَّ لَكُمۡ لَيۡلَةَ ٱلصِّيَامِ ٱلرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَآئِكُمۡۚ هُنَّ لِبَاسٞ لَّكُمۡ وَأَنتُمۡ لِبَاسٞ لَّهُنَّۗ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمۡ كُنتُمۡ تَخۡتَانُونَ أَنفُسَكُمۡ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡ وَعَفَا عَنكُمۡۖ فَٱلۡـَٰٔنَ بَٰشِرُوهُنَّ وَٱبۡتَغُواْ مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمۡۚ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِۖ ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِۚ وَلَا تُبَٰشِرُوهُنَّ وَأَنتُمۡ عَٰكِفُونَ فِي ٱلۡمَسَٰجِدِۗ تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَقۡرَبُوهَاۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ ءَايَٰتِهِۦ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ ﴾
[البَقَرَة: 187]

Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate kumcha

❮ Previous Next ❯

ترجمة: أحل لكم ليلة الصيام الرفث إلى نسائكم هن لباس لكم وأنتم لباس, باللغة السواحيلية

﴿أحل لكم ليلة الصيام الرفث إلى نسائكم هن لباس لكم وأنتم لباس﴾ [البَقَرَة: 187]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Amewahalalishia Mwenyezi Mungu masiku ya mwezi wa Ramadhani kuwaingilia wake zenu. Wao ni sitara na hifadhi kwenu, na nyinyi ni sitara na hifadhi kwao. Anajua Mwenyezi Mungu kwamba nyinyi mulikuwa mkizidhiki nafsi zenu kwa kuenda kinyume na yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliyaharimisha kwenu ya kuwaingilia wanawake baada ya Isha katika masiku ya kufunga- hilo lilikuwa mwanzo wa Uislamu-, Mwenyezi Mungu Alikubali toba yenu na Akawatolea nafasi kwa hili jambo. Basi sasa waingilieni na mtafute kile Alichowakadiria Mwenyezi Mungu, miongoni mwa watoto, na kuleni na kunyweni mpaka ujitokeze kwenu mwangaza wa asubuhi utengane na weusi wa usiku kwa kujitokeza alfajiri ya kweli. Kisha kamilisheni kufunga kwa kujizuia na venye kutangua mpaka kuingia usiku kwa kutwa jua. Wala musiwaingilie wake zenu, au kufanya kitu cha kusababisha kuwaingilia, iwapo muko kwenye itikafu misikitini, sababu hilo laharibu itikafu- nako ni kukaa msikitini kwa muda maalumu kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka-. Hukumu hizo, ambazo mwenyezi Mungu Amezifanya ni Sheria kwenu, ndiyo mipaka Yake itenganishayo kati ya halali na haramu. Basi msiikaribie, ili msije mkaingia katika haramu. Kwa mfano wa ubainifu huu ulio wazi, Mwenyezi Mungu Anazifafanua aya Zake na hukumu Zake kwa watu, ili wamche na kumuogopa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek