Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 231 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَإِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَبَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمۡسِكُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٖۚ وَلَا تُمۡسِكُوهُنَّ ضِرَارٗا لِّتَعۡتَدُواْۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَقَدۡ ظَلَمَ نَفۡسَهُۥۚ وَلَا تَتَّخِذُوٓاْ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ هُزُوٗاۚ وَٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَمَآ أَنزَلَ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡحِكۡمَةِ يَعِظُكُم بِهِۦۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 231]
﴿وإذا طلقتم النساء فبلغن أجلهن فأمسكوهن بمعروف أو سرحوهن بمعروف ولا تمسكوهن﴾ [البَقَرَة: 231]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Pindi mtakapowataliki wanawake wakakaribia siku za kumaliza eda lao, basi warejeeni hali ya kuwa nia zenu ni kuwatekelezea haki zao kwa njia nzuri, kisheria na kidesturi, au waacheni mpaka eda lao limalizike. Na kueni na hadhari, isije ikawa kuwarejea ni kwa lengo la kuwadhuru kwa kuwafanyia uadui katika haki zao. Na yoyote atakayelifanya hilo, ameshaidhulumu nafsi yake kwa kustahiki mateso. Na wala msizifanye aya za Mwenyezi Mungu na hukumu Zake kuwa ni mchezo na upuzi. Nakumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu, kwa kuwafanya Waislamu na kuwafafanulia hukumu Zake. Na yakumbukeni yale Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, ya Qur’ani na mafundisho ya Mtume Wake. Na mshukuruni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa neema hizi zilzo kubwa. Mwenyezi Mungu Anawakumbusha hayo na Anawatisha msende kinyume nayo. Basi, mcheni Mwenyezi Mungu na mumlindize. Na mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, hapana kitu chenye kufichika Kwake, na Atamlipa kila mmoja kwa anayostahiki alipwe |