×

Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakawacha wake, na wausie kwa 2:240 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:240) ayat 240 in Swahili

2:240 Surah Al-Baqarah ayat 240 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 240 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنكُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٰجٗا وَصِيَّةٗ لِّأَزۡوَٰجِهِم مَّتَٰعًا إِلَى ٱلۡحَوۡلِ غَيۡرَ إِخۡرَاجٖۚ فَإِنۡ خَرَجۡنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِي مَا فَعَلۡنَ فِيٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعۡرُوفٖۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 240]

Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakawacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumba. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hapana ubaya kwenu kwa waliyo jifanyia wenyewe kwa mujibu wa Sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima

❮ Previous Next ❯

ترجمة: والذين يتوفون منكم ويذرون أزواجا وصية لأزواجهم متاعا إلى الحول غير إخراج, باللغة السواحيلية

﴿والذين يتوفون منكم ويذرون أزواجا وصية لأزواجهم متاعا إلى الحول غير إخراج﴾ [البَقَرَة: 240]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na waume wanaofariki na wakaacha wake baada yao, inawalazimu waume hao wawekee wasia hao wake zao kwamba waliwazwe mwaka mzima kuanzia siku ya kufariki, kwa kupewa Makao katika nyumba ya mume, bila ya kutolewa na mawarithi kwa muda wa mwaka. Hilo likiwa ni maliwazo kwa yule mke na ni wema kwa aliyefariki. Na iwapo wanawake hao waliofiliwa watatoka, kwa hiyari yao kabla mwaka kumalizika, basi hamna makosa, nyinyi warithi, katika hilo. Pia, hakuna makosa kwa hao wanawake kwa kitendo chao cha halali walichojifanyia nafsi zao. Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika amri Zake na Makatazo Yake. Aya hii, hukumu zake zimeondolewa kwa neno Lake Mwenyezi Mungu Aliyetukaka, «Na wale wanaofariki kati yenu na wakaacha wake zao, (Basi wake hao) wajizuie nafsi zao miezi mine na siku kumi»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek