×

Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni 2:261 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:261) ayat 261 in Swahili

2:261 Surah Al-Baqarah ayat 261 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 261 - البَقَرَة - Page - Juz 3

﴿مَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتۡ سَبۡعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنۢبُلَةٖ مِّاْئَةُ حَبَّةٖۗ وَٱللَّهُ يُضَٰعِفُ لِمَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ ﴾
[البَقَرَة: 261]

Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua

❮ Previous Next ❯

ترجمة: مثل الذين ينفقون أموالهم في سبيل الله كمثل حبة أنبتت سبع سنابل, باللغة السواحيلية

﴿مثل الذين ينفقون أموالهم في سبيل الله كمثل حبة أنبتت سبع سنابل﴾ [البَقَرَة: 261]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na miongoni mwa vitu bora zaidi vinavyowanufaisha Waumini ni kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na mfano wa Waumini wenye kutoa mali yao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa mbegu iliyopandwa kwenye ardhi nzuri, muda si muda ikatoa mte wenye sehemu saba. Kila sehemu ikatoa suke moja na kila suke likawa na mbegu mia. Na Mwenyezi Mungu Anamuongezea thawabu anayemtaka, kulingana na kadiri ya Imani aliyonayo yule mtoaji na ikhlasi yake iliyo timamu.Na fadhila za Mwenyezi Mungu zimeenea, na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mjuzi wa yule anayestahiki kuzipata, ni Mwenye kuchungulia nia za waja Wake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek