Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 262 - البَقَرَة - Page - Juz 3
﴿ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ لَا يُتۡبِعُونَ مَآ أَنفَقُواْ مَنّٗا وَلَآ أَذٗى لَّهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ﴾
[البَقَرَة: 262]
﴿الذين ينفقون أموالهم في سبيل الله ثم لا يتبعون ما أنفقوا منا﴾ [البَقَرَة: 262]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wale ambao wanatoa mali yao katika jihadi na aina mbali-mbali za kheri, kisha wasifuatishe, yale waliyoyatoa ya kheri, kwa kumsumbulia waliyempa wala kumkera, kwa neno au kitendo, kwa kumhisisha kuwa wamemfadhili, watapata thawabu kubwa mbele ya Mola wao na hawatakuwa na kicho kuhusu mustakbala wao wa Akhera wala hawatahuzunika juu ya kitu chochote kilichowapita wasikipate katika ulimwengu |