Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 83 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ لَا تَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَانٗا وَذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَقُولُواْ لِلنَّاسِ حُسۡنٗا وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ ثُمَّ تَوَلَّيۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنكُمۡ وَأَنتُم مُّعۡرِضُونَ ﴾
[البَقَرَة: 83]
﴿وإذ أخذنا ميثاق بني إسرائيل لا تعبدون إلا الله وبالوالدين إحسانا وذي﴾ [البَقَرَة: 83]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Kumbukeni, enyi Wana wa Isrāīl, tulipochukua ahadi ya mkazo kwenu kwamba mtamuabudu Mwenyezi Mungu peke Yake Asiye na mshirika, muwafanyie wema wazazi wawili na watoto waliofiliwa na baba zao nao wako chini ya umri wa kubaleghe na masikini na kwamba muwaambie watu maneno mazuri, pamoja na kusimamisha Swala na kutoa Zaka. Kisha mkageuka na mkavunja ahadi, isipokuwa wachache katika nyinyi waliosimama imara juu yake. Na nyinyi bado mnaendelea kugeuka kwenu |