Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 87 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَقَفَّيۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ بِٱلرُّسُلِۖ وَءَاتَيۡنَا عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدۡنَٰهُ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِۗ أَفَكُلَّمَا جَآءَكُمۡ رَسُولُۢ بِمَا لَا تَهۡوَىٰٓ أَنفُسُكُمُ ٱسۡتَكۡبَرۡتُمۡ فَفَرِيقٗا كَذَّبۡتُمۡ وَفَرِيقٗا تَقۡتُلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 87]
﴿ولقد آتينا موسى الكتاب وقفينا من بعده بالرسل وآتينا عيسى ابن مريم﴾ [البَقَرَة: 87]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tulimpa Mūsā Taurati, na kuwaleta baada yake Mitume wengine miongoni mwa Wana wa Isrāīl. Na tulimpa ' Īsā mwana wa Maryam miujiza iliyo wazi na kumtilia nguvu kwa Jibrili, amani imshukie. Kwani nyinyi mumekuwa kila Mtume anapowajia na Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, usiolingana na matamanio yenu, mnamfanyia kiburi, wengine mkiwakanusha na wengine mkiwaua |