Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 88 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَقَالُواْ قُلُوبُنَا غُلۡفُۢۚ بَل لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفۡرِهِمۡ فَقَلِيلٗا مَّا يُؤۡمِنُونَ ﴾
[البَقَرَة: 88]
﴿وقالوا قلوبنا غلف بل لعنهم الله بكفرهم فقليلا ما يؤمنون﴾ [البَقَرَة: 88]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wana wa Isrāīl walisema kumwambia Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, “Nyoyo zetu zimezibwa kwa namna ambayo maneno yako hayapenyezi ndani yake.” Mambo si kama walivyodai. Bali nyonyo zao zimelaaniwa, zimepigwa muhuri juu ya hiyo laana. Na wao wamefukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kukanusha kwao. Wao hawaamini isipokuwa imani chache isiyowafaa |