Quran with Swahili translation - Surah Ta-Ha ayat 114 - طه - Page - Juz 16
﴿فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّۗ وَلَا تَعۡجَلۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مِن قَبۡلِ أَن يُقۡضَىٰٓ إِلَيۡكَ وَحۡيُهُۥۖ وَقُل رَّبِّ زِدۡنِي عِلۡمٗا ﴾
[طه: 114]
﴿فتعالى الله الملك الحق ولا تعجل بالقرآن من قبل أن يقضى إليك﴾ [طه: 114]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ameepukana Mwenyezi Mungu, kutakata ni Kwake, na Amekuwa juu na ametakasika na kila upungufu, Aliye Mfalme Ambaye mamlaka Yake yamemtendesha nguvu kila mfalme na mjeuri, Mwenye kuendesha kila kitu, Ambaye Yeye Ndiye ukweli, na agizo Lake ni kweli, na onyo Lake ni kweli, na kila kitu kinachotoka Kwake ni kweli. Na usifanye haraka, ewe Mtume, ya kushindana na Jibrili katika kuipokea Qur’ani kabla hajaimaliza, na useme, «Mola wangu! Niongezee elimu juu ya ile uliyonifundisha.» |