Quran with Swahili translation - Surah Ta-Ha ayat 64 - طه - Page - Juz 16
﴿فَأَجۡمِعُواْ كَيۡدَكُمۡ ثُمَّ ٱئۡتُواْ صَفّٗاۚ وَقَدۡ أَفۡلَحَ ٱلۡيَوۡمَ مَنِ ٱسۡتَعۡلَىٰ ﴾
[طه: 64]
﴿فأجمعوا كيدكم ثم ائتوا صفا وقد أفلح اليوم من استعلى﴾ [طه: 64]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi vithibitisheni vitimbi vyenu na muwe na nia moja juu ya hilo pasi na kutengana kati yenu, kisha njooni mkiwa ni safu moja na mvirushe vilivyomo mikononi mwenu kwa mara moja ili muyashangaze macho ya watu na muushinde uchawi wa Mūsā na ndugu yake. Na kwa kweli, leo amepata matakwa yake yule atakayekuwa juu ya mwenzake akamshinda na akambana.» |