Quran with Swahili translation - Surah Ta-Ha ayat 96 - طه - Page - Juz 16
﴿قَالَ بَصُرۡتُ بِمَا لَمۡ يَبۡصُرُواْ بِهِۦ فَقَبَضۡتُ قَبۡضَةٗ مِّنۡ أَثَرِ ٱلرَّسُولِ فَنَبَذۡتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتۡ لِي نَفۡسِي ﴾
[طه: 96]
﴿قال بصرت بما لم يبصروا به فقبضت قبضة من أثر الرسول فنبذتها﴾ [طه: 96]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sāmirīy akasema, «Nilimuona ambaye hawakumuona, naye ni Jibrili, amani imshukiye, juu ya farasi, wakati walipotoka baharini na Fir'awn akazamishwa na askari wake, hapo niliteka kwa kitanga changu cha mkono mchanga wa athari ya kwato za farasi wa Jibrili nikaurusha kwenye pambo ambalo kwalo nimetengeneza kigombe, kikawa ni kigombe chenye mwili, chenye kutoa sauti ya ng’ombe, na kikawa ni kisirani na mtihani. Kufanya hivyo ndivyo nafsi yangu inayoamrisha maovu ilivyonipambia.» |