Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 26 - النور - Page - Juz 18
﴿ٱلۡخَبِيثَٰتُ لِلۡخَبِيثِينَ وَٱلۡخَبِيثُونَ لِلۡخَبِيثَٰتِۖ وَٱلطَّيِّبَٰتُ لِلطَّيِّبِينَ وَٱلطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَٰتِۚ أُوْلَٰٓئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَۖ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ ﴾
[النور: 26]
﴿الخبيثات للخبيثين والخبيثون للخبيثات والطيبات للطيبين والطيبون للطيبات أولئك مبرءون مما يقولون﴾ [النور: 26]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kila kiovu miongoni mwa wanaume na wanawake, maneno na vitendo, kinalingana na kiovu na kinaoana nacho. Na kila kizuri miongoni mwa wanaume na wanawake, maneno na vitendo, kinalingana na kizuri na kinaoana nacho. Na wanaume wazuri na wanawake wazuri ni wenye kutakaswa na uovu wanaowasingizia nao wale waovu. Watapata kutoka kwa Mwenyezi Mungu msamaha utakaoyafinika madhambi yote na riziki njema Peponi |