Quran with Swahili translation - Surah Al-Furqan ayat 6 - الفُرقَان - Page - Juz 18
﴿قُلۡ أَنزَلَهُ ٱلَّذِي يَعۡلَمُ ٱلسِّرَّ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّهُۥ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا ﴾
[الفُرقَان: 6]
﴿قل أنـزله الذي يعلم السر في السموات والأرض إنه كان غفورا رحيما﴾ [الفُرقَان: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Kwa hakika Aliyeiteremsha Qur’ani ni Mwenyezi Mungu Ambaye ujuzi Wake umevizunguka vilivyoko mbinguni na ardhini. Kwa hakika Yeye ni Msamehefu sana kwa waliotubia kutokana na madhambi na maasia, ni Mwenye huruma kwao kwa kuwa hakufanya haraka ya kuwatesa.» |