Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 45 - النَّمل - Page - Juz 19
﴿وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ فَإِذَا هُمۡ فَرِيقَانِ يَخۡتَصِمُونَ ﴾
[النَّمل: 45]
﴿ولقد أرسلنا إلى ثمود أخاهم صالحا أن اعبدوا الله فإذا هم فريقان﴾ [النَّمل: 45]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tulimtumiliza kwa watu wa Thamūd ndugu yao Ṣāliḥ kwamba: Mpwekesheni Mwenyezi Mungu na musimchukue mungu mwingine mukamuabudu pamoja na Yeye. Alipowajia Ṣāliḥ kuwalingania kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumuabudu Peke Yake, watu wake walikuwa mapote mawili: mojawapo ya mapote mawili lilimuamini na lingine liliukanusha ulinganizi wake, kila mmoja kati ya watu wa mapote hayo mawili alikuwa akidai kwamba haki iko pamoja na yeye |