Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 44 - النَّمل - Page - Juz 19
﴿قِيلَ لَهَا ٱدۡخُلِي ٱلصَّرۡحَۖ فَلَمَّا رَأَتۡهُ حَسِبَتۡهُ لُجَّةٗ وَكَشَفَتۡ عَن سَاقَيۡهَاۚ قَالَ إِنَّهُۥ صَرۡحٞ مُّمَرَّدٞ مِّن قَوَارِيرَۗ قَالَتۡ رَبِّ إِنِّي ظَلَمۡتُ نَفۡسِي وَأَسۡلَمۡتُ مَعَ سُلَيۡمَٰنَ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[النَّمل: 44]
﴿قيل لها ادخلي الصرح فلما رأته حسبته لجة وكشفت عن ساقيها قال﴾ [النَّمل: 44]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Akaambiwa, «Ingia kwenye jumba.» na ukumbi wake ulikuwa wa ukoa, chini yake palikuwa na maji. Alipouona ukumbi alidhania ni maji yanayopiga mawimbi, na akafunua miguu yake ili kuingia majini. Sulaymān akamwambia, «Huo ni ukumbi laini wa ukoa ulio safi na maji yako chini yake.» Akatambua ukubwa wa ufalme wa Sulaymān na akasema, «Mola wangu! Nimeidhulumu nafsi yangu kwa ushirikina niliokuwa nao, na nimesalimu amri kwa kumfuata Sulaymān kwa kuingia kwenye dini ya Mola wa viumbe wote.» |