Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 63 - النَّمل - Page - Juz 20
﴿أَمَّن يَهۡدِيكُمۡ فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ وَمَن يُرۡسِلُ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦٓۗ أَءِلَٰهٞ مَّعَ ٱللَّهِۚ تَعَٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ﴾
[النَّمل: 63]
﴿أمن يهديكم في ظلمات البر والبحر ومن يرسل الرياح بشرا بين يدي﴾ [النَّمل: 63]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, kuviabudu vile mnavyomshirikisha navyo Mwenyezi Mungu ni bora au Yule Anayewaongoza katika giza la bara na bahari mnapopotea na njia ikawa na giza kwenu, Ambaye Anapeleka upepo wenye kutoa bishara njema ya kile ambacho Mwenyezi Mungu Anawarehemu waja Wake kwacho, nacho ni mvua yenye kuhuisha ardhi iliyokufa? Je, kuna muabudiwa yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu anayewafanyia chochote katika hayo mkamuomba badala yake? Ameepukana Mwenyezi Mungu na kutakasika na hivyo ambavyo wao wanamshirikisha navyo asiyekuwa Yeye |