Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 146 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيّٖ قَٰتَلَ مَعَهُۥ رِبِّيُّونَ كَثِيرٞ فَمَا وَهَنُواْ لِمَآ أَصَابَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَمَا ضَعُفُواْ وَمَا ٱسۡتَكَانُواْۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلصَّٰبِرِينَ ﴾
[آل عِمران: 146]
﴿وكأين من نبي قاتل معه ربيون كثير فما وهنوا لما أصابهم في﴾ [آل عِمران: 146]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wengi kati ya Mitume waliotangulia, walipigana pamoja nao makundi mengi ya watu waliowafuata. Hawakudhoofika kwa yale yaliyowapata ya majaraha au mauaji, kwani hayo yalikuwa katika njia ya Mola wao. Wala hawakulemewa wala hawakumnyenyekea adui yao, bali walisubiri kwa yaliyowapata. Na Mwenyezi Mungu Anawapenda wenye kusubiri |