Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 145 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِ كِتَٰبٗا مُّؤَجَّلٗاۗ وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَا وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلۡأٓخِرَةِ نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَاۚ وَسَنَجۡزِي ٱلشَّٰكِرِينَ ﴾
[آل عِمران: 145]
﴿وما كان لنفس أن تموت إلا بإذن الله كتابا مؤجلا ومن يرد﴾ [آل عِمران: 145]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakuna yoyote atakayekufa isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na makadirio Yake na mpaka aufikishe muda ambao Mwenyezi Mungu Amempangia. Hayo ni maandishi yaliyopangiwa wakati. Na yoyote ambaye kwa vitendo vyake anataka manufaa ya duniani, tutampa tulichomgawia cha riziki, na hatakuwa na fungu lolote kesho Akhera. Na yoyote ambaye anataka kwa vitendo vyake malipo ya Mwenyezi Mungu huko Akhera , tutampa kile alichokitaka na tutampa malipo yake kamili pamoja na fungu lake duniani la riziki alilogawiwa. Kwani huyu kwa utiifu wake na jihadi yake ametushukuru; na wenye kushukuru tutawalipa mema |