×

Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio kufuru na wakawasema ndugu zao 3:156 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:156) ayat 156 in Swahili

3:156 Surah al-‘Imran ayat 156 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 156 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَقَالُواْ لِإِخۡوَٰنِهِمۡ إِذَا ضَرَبُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَوۡ كَانُواْ غُزّٗى لَّوۡ كَانُواْ عِندَنَا مَا مَاتُواْ وَمَا قُتِلُواْ لِيَجۡعَلَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ حَسۡرَةٗ فِي قُلُوبِهِمۡۗ وَٱللَّهُ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ﴾
[آل عِمران: 156]

Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio kufuru na wakawasema ndugu zao walipo safiri katika nchi au walipo kuwa vitani: Wangeli kuwa kwetu wasingeli kufa na wasingeli uwawa. Ili Mwenyezi Mungu afanye hayo kuwa ni majuto katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona myatendayo

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا لا تكونوا كالذين كفروا وقالوا لإخوانهم إذا ضربوا في, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا لا تكونوا كالذين كفروا وقالوا لإخوانهم إذا ضربوا في﴾ [آل عِمران: 156]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, msijifananishe na makafiri ambao hawamuamini Mola wao. Kwani wao huwaambia ndugu zao, miongoni mwa makafiri, wanapotoka kwenda kutafuta maisha yao katika ardhi au wanapokuwa pamoja na wapiganaji, wakafa au wakauawa, «Lau kama hawa hawangetoka wala hawangepigana na wakabakia pamoja na sisi, hawangekufa wala hawangeuawa.» Neno hili linawaongezea machungu, maudhiko na majuto yanayobakia katika nyoyo zao. Ama Waumini, wao wanajua kwamba hili limetokana na kadara ya Mwenyezi Mungu, ndipo Mwenyezi Mungu Huziongoza nyoyo zao na Huwasahilishia misiba. Na Mwenyezi Mungu Anambakisha hai yule Aliyemkadiria kuishi, hata kama ni msafiri au ni mpiganaji. Na Anamfisha yule ambaye muda wake wa kuishi umekoma, hata kama ni mkazi wa mji. Na Mwenyezi Mungu kwa kila mlifanyalo ni Mwenye kuliona, na Atawalipa kwalo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek