Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 166 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿وَمَآ أَصَٰبَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِ فَبِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[آل عِمران: 166]
﴿وما أصابكم يوم التقى الجمعان فبإذن الله وليعلم المؤمنين﴾ [آل عِمران: 166]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na yale yaliyotokea kwenu ya majaraha au ya mauaji katika vita vya Uhud, siku ulipokutana mkusanyiko wa Waumini na mkusanyiko wa washirikina, na ukawa ushindi, mwanzo wa vita, ni wa Waumini kisha, mara ya pili, ukwa ni wa washirikina, yote hayo yalikuwa kwa uamuzi wa Mwenyezi Mungu na mpango Wake, ili yajitokeze yale Aliyoyajua Mwenyezi Mungu tangu kale, ili Awapambanue Waumini wa kweli miongoni mwenu |