Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 30 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿يَوۡمَ تَجِدُ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ مِنۡ خَيۡرٖ مُّحۡضَرٗا وَمَا عَمِلَتۡ مِن سُوٓءٖ تَوَدُّ لَوۡ أَنَّ بَيۡنَهَا وَبَيۡنَهُۥٓ أَمَدَۢا بَعِيدٗاۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفۡسَهُۥۗ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ ﴾
[آل عِمران: 30]
﴿يوم تجد كل نفس ما عملت من خير محضرا وما عملت من﴾ [آل عِمران: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na katika Siku ya Kiyama, Siku ya Malipo, kila nafsi italikuta jema lolote ililolifanya linaingojea likiwa limeongezwa ili ilipwe nalo. Na pia baya iliolifanya italikuta linaingojea vilevile, hapo itatamani lau ilikuwa baina yake na hilo tendo baya zama zirefu. Basi jitayarisheni kwa Siku hii, na muogope mateso ya Mola Aliye Jabari. Na pamoja na ukali wa mateso Yake, Yeye, Aliyetakata na sifa za upungufu, ni Msifika kwa ukamilifu wa huruma kwa waja |