×

Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye 3:7 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:7) ayat 7 in Swahili

3:7 Surah al-‘Imran ayat 7 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 7 - آل عِمران - Page - Juz 3

﴿هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ مِنۡهُ ءَايَٰتٞ مُّحۡكَمَٰتٌ هُنَّ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ وَأُخَرُ مُتَشَٰبِهَٰتٞۖ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمۡ زَيۡغٞ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَٰبَهَ مِنۡهُ ٱبۡتِغَآءَ ٱلۡفِتۡنَةِ وَٱبۡتِغَآءَ تَأۡوِيلِهِۦۖ وَمَا يَعۡلَمُ تَأۡوِيلَهُۥٓ إِلَّا ٱللَّهُۗ وَٱلرَّٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ يَقُولُونَ ءَامَنَّا بِهِۦ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ رَبِّنَاۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ ﴾
[آل عِمران: 7]

Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili

❮ Previous Next ❯

ترجمة: هو الذي أنـزل عليك الكتاب منه آيات محكمات هن أم الكتاب وأخر, باللغة السواحيلية

﴿هو الذي أنـزل عليك الكتاب منه آيات محكمات هن أم الكتاب وأخر﴾ [آل عِمران: 7]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Yeye Peke Yake Ndiye Ambaye Aliyekuteremshia Qur’ani ambayo katika hiyo kuna aya zenye maana yaliyo wazi; hizo ndizo msingi wa Kitabu ambao unategemewa ikitokea tashwishi, na ambao chochote kinachohalifiana nao kinarudishwa na kuoanishwa nao. Na katika hiyo kuna aya zingine mutashabihat: zinazoleta tashwishi kwa kuwa zinabeba zaidi ya maana mamoja, kwa namna ambayo haiwezekani kujuwa maana iliyokusudiwa isipokuwa kwa kuziambatanisha na muhkam: aya zenye maana yaliyo wazi. Basi wenye nyoyo zenye ugonjwa zilizopotoka, kwa ubaya wa nia zao, huzifuata hizi aya zenye tashwishi peke yake, ili kutia tashwishi kwa watu kwa lengo la kuwapoteza kwa kuzifasiri kuambatana na madhehebu yao yaliyo batili. Ilihali hakuna ajuwaye uhakika wa maana ya aya hizi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wale waliovama kwenye elimu wanasema, «Tumeiamini hii Qur’ani, kwani yote imetujia kutoka kwa Mola wetu kwa ulimi wa Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,.» na wanairudisha yenye tashwishi katika Qur’ani na kuiyoanisha na iliyo wazi yake. Hakika ni kwamba wanaoyafahamu na kuyazingatia maana kama ilivyo sahihi ipasavyo ni wale wenye akili timamu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek