Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 98 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعۡمَلُونَ ﴾
[آل عِمران: 98]
﴿قل ياأهل الكتاب لم تكفرون بآيات الله والله شهيد على ما تعملون﴾ [آل عِمران: 98]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliepewa vitabu kati ya Mayahudi na Wanaswara, «Kwa nini mnazikanusha hoja za Mwenyezi Mungu zinazojulisha kwamba dini ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu na mnayakanusha yaliyomo kwenye vitabu vyenu miongoni mwa dalili na hoja juu ya hilo hali ya kuwa nyinyi mnajua? Na Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya kitendo chenu mnachokifanya.» Katika haya, pana makemeo na ahadi ya adhabu kwao |