×

Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye 3:97 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:97) ayat 97 in Swahili

3:97 Surah al-‘Imran ayat 97 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 97 - آل عِمران - Page - Juz 4

﴿فِيهِ ءَايَٰتُۢ بَيِّنَٰتٞ مَّقَامُ إِبۡرَٰهِيمَۖ وَمَن دَخَلَهُۥ كَانَ ءَامِنٗاۗ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلۡبَيۡتِ مَنِ ٱسۡتَطَاعَ إِلَيۡهِ سَبِيلٗاۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[آل عِمران: 97]

Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: فيه آيات بينات مقام إبراهيم ومن دخله كان آمنا ولله على الناس, باللغة السواحيلية

﴿فيه آيات بينات مقام إبراهيم ومن دخله كان آمنا ولله على الناس﴾ [آل عِمران: 97]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Katika Nyumba hii kuna alama waziwazi ya kwamba hiyo ni katika ujenzi wa Ibrāhīm na kwamba Mwenyezi Mungu ameitukuza na kuipa heshima. Kati ya alama hizo ni Maqām ya Ibrāhīm, amani imshukie, nayo ni lile jiwe ambalo alikuwa akisimama juu yake wakati alipokuwa akiziinua nguzo za Alkaba, yeye na mwanawe Ismā'īl. Na yoyote mwenye kuingia Nyumba hii atapata amani ya nafsi yake, hapana yoyote atakayemkusudia kwa uovu. Na Mwenyezi Mungu Amewajibisha kwa mwenye uwezo katika watu, popote atakapokuwa kuiendea nyumba hii ili kutekeleza matendo ya Hija. Na yoyote mwenye kuikanusha faradhi ya Hija, basi huyo amekufuru. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi naye, Hana haja ya hija yake wala amali yake na wala Hana haja na viumbe vyake vyote
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek