Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 21 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦٓ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٰجٗا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَكُم مَّوَدَّةٗ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ ﴾
[الرُّوم: 21]
﴿ومن آياته أن خلق لكم من أنفسكم أزواجا لتسكنوا إليها وجعل بينكم﴾ [الرُّوم: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa alama zenye kuonyesha ukubwa Wake na ukamilifu wa uweza wake ni kuwa Amewaumba wake kwa ajili yenu kutokana na jinsi yenu, enyi wanaume, ili nafsi zenu zijitulize kwao na ziburudike, na Akatia mapenzi na huruma baina ya mwanamke na mumewe. Hakika katika uumbaji huo wa Mwenyezi Mungu pana alama zenye kuonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu na kupwekeka Kwake kwa watu wenye kufikiria na kuzingatia |