Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 22 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦ خَلۡقُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَٰفُ أَلۡسِنَتِكُمۡ وَأَلۡوَٰنِكُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡعَٰلِمِينَ ﴾
[الرُّوم: 22]
﴿ومن آياته خلق السموات والأرض واختلاف ألسنتكم وألوانكم إن في ذلك لآيات﴾ [الرُّوم: 22]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu ni uumbaji mbingu na kuwa juu kwake bila ya nguzo, na uumbaji ardhi ikiwa imekunjuka na kupanuka, na kutafautiana lugha zenu na kuwa mbalimbali rangi zenu. Hakika katika hayo kuna mazingatio kwa kila mwenye elimu na busara |