Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 24 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦ يُرِيكُمُ ٱلۡبَرۡقَ خَوۡفٗا وَطَمَعٗا وَيُنَزِّلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَيُحۡيِۦ بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ ﴾
[الرُّوم: 24]
﴿ومن آياته يريكم البرق خوفا وطمعا وينـزل من السماء ماء فيحيي به﴾ [الرُّوم: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa dalili za uweza Wake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake ni kuwaonyesha umeme, mkaogopa vimondo na mkawa na matumaini ya mvua, na Anateremsha mvua kutoka mawinguni ikahuisha ardhi baada ya kuwa katika hali ya ukame na ukavu. Hakika katika hayo kuna dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu na ukubwa wa hekima Yake na wema Wake kwa kila Mwenye akili ya kujiongoza |