Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 23 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦ مَنَامُكُم بِٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَٱبۡتِغَآؤُكُم مِّن فَضۡلِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ ﴾
[الرُّوم: 23]
﴿ومن آياته منامكم بالليل والنهار وابتغاؤكم من فضله إن في ذلك لآيات﴾ [الرُّوم: 23]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa dalili za uweza huu ni kuwa Mwenyezi Mungu Amewawekea usingizi uwe ni mapumziko kwenu ya usiku au mchana, kwani katika kulala yanapatikana mapumziko na kuondokewa na machovu, na Amewawekea mchana ambapo ndani yake mnaenda huku na kule kutafuta riziki. Hakika katika hayo kuna dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu na upitishaji matakwa Yake kwa watu wanaosikia mawaidha usikiaji wa kutia akilini, kufikiria na kuzingatia |