Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 38 - الأحزَاب - Page - Juz 22
﴿مَّا كَانَ عَلَى ٱلنَّبِيِّ مِنۡ حَرَجٖ فِيمَا فَرَضَ ٱللَّهُ لَهُۥۖ سُنَّةَ ٱللَّهِ فِي ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلُۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ قَدَرٗا مَّقۡدُورًا ﴾
[الأحزَاب: 38]
﴿ما كان على النبي من حرج فيما فرض الله له سنة الله﴾ [الأحزَاب: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Haikuwa ni dhambi kwa Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, katika kile Alichomhalalishia Mwenyezi Mungu cha kumuoa mke wa mwanawe wa kujibandika baada ya kumuacha, kama vile alivyowahalalishia hilo Manabii kabla yake yeye, ni mwenendo uliowekwa na Mwenyezi Mungu kwa wale waliopita kabla. Na kwa kweli, amri ya Mwenyezi Mungu ni mpango uliokadiriwa , hauna budi kutokea |