Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 52 - الأحزَاب - Page - Juz 22
﴿لَّا يَحِلُّ لَكَ ٱلنِّسَآءُ مِنۢ بَعۡدُ وَلَآ أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجٖ وَلَوۡ أَعۡجَبَكَ حُسۡنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتۡ يَمِينُكَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ رَّقِيبٗا ﴾
[الأحزَاب: 52]
﴿لا يحل لك النساء من بعد ولا أن تبدل بهن من أزواج﴾ [الأحزَاب: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Haifai kwako kuwaoa wanawake baada ya wake zako walio mama wa Waumini, na usiwaache wao ukawaoa wengine badala yao, kwa kuwakirimu na kushukuru mazuri waliyoyatenda ya kumchagua Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Nyumba ya Akhera, hata kama utavutiwa na uzuri wa hao wanawake wengine, isipokuwa kile ambacho mkono wako wa kulia umemiliki, miongoni mwa wajakazi, kwani hao ni halali kwako. Na Mwenyezi Mungu anakiona kila kitu, hakuna chochote kilicho nje ya ujuzi Wake |