Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahzab ayat 72 - الأحزَاب - Page - Juz 22
﴿إِنَّا عَرَضۡنَا ٱلۡأَمَانَةَ عَلَى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱلۡجِبَالِ فَأَبَيۡنَ أَن يَحۡمِلۡنَهَا وَأَشۡفَقۡنَ مِنۡهَا وَحَمَلَهَا ٱلۡإِنسَٰنُۖ إِنَّهُۥ كَانَ ظَلُومٗا جَهُولٗا ﴾
[الأحزَاب: 72]
﴿إنا عرضنا الأمانة على السموات والأرض والجبال فأبين أن يحملنها وأشفقن منها﴾ [الأحزَاب: 72]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sisi tuliiorodhesha amana- ambayo Mwenyezi Mungu Amewapatia waliokalifishwa na Sheria waitunze, nayo ni kufuata maamrisho na kujiepusha na makatazo- kwa mbingu, ardhi na majabali, vikakataa kuibeba na vikaogopa visiweze kusimama kuitekeleza, na akaibeba binadamu na akashikamana nayo pamoja na udhaifu Wake. Hakika yeye ni mwingi wa udhalimu na ujinga wa nafsi yake |