Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 136 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِن قَبۡلُۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱللَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا ﴾
[النِّسَاء: 136]
﴿ياأيها الذين آمنوا آمنوا بالله ورسوله والكتاب الذي نـزل على رسوله والكتاب﴾ [النِّسَاء: 136]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, endeleeni kwenye msimamo mlionao wa kumuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Imani thabiti, kumuamini Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na kuwatii wao wawili, kuiamini Qur’ani Aliyoiteremsha kwake na kuviamini vitabu vyote Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume. Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Malaika Wake waliotukuzwa, vitabu Vyake Alivyoviteremsha ili kuwaongoza viumbe Wake, Mitume Wake Aliowachagua kufikisha ujumbe Wake na Siku ya Mwisho ambayo watu katika siku hiyo watafufuka baada ya kufa ili waorodheshwe na wahesabiwe, atakuwa ametoka kwenye Dini na atakuwa yuko mbali sana na njia ya haki |