Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 35 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَإِنۡ خِفۡتُمۡ شِقَاقَ بَيۡنِهِمَا فَٱبۡعَثُواْ حَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهِۦ وَحَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصۡلَٰحٗا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيۡنَهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرٗا ﴾
[النِّسَاء: 35]
﴿وإن خفتم شقاق بينهما فابعثوا حكما من أهله وحكما من أهلها إن﴾ [النِّسَاء: 35]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mkijua, enyi wasimamizi wa mume na mke, kuwa kuna ugomvi baina yao unaopelekea kutengana, wapelekeeni mwamuzi muadilifu wa upande wa mume na mwamuzi muadilifu wa upande wa mke, ili watazame na kutoa uamuzi wenye maslahi ya wao wawili. Na kwa kuwa wale waamuzi wawili wana hamu ya kupatanisha na wanatumia njia nzuri, Mwenyezi Mungu Atawatilia taufiki baina ya mume na mke. Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, hakuna chochote kinachofichamana Kwake kuhusu mambo ya waja Wake, ni Mtambuzi wa yaliyomo ndani ya nafsi zao |