×

Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao 4:34 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:34) ayat 34 in Swahili

4:34 Surah An-Nisa’ ayat 34 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 34 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿ٱلرِّجَالُ قَوَّٰمُونَ عَلَى ٱلنِّسَآءِ بِمَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ وَبِمَآ أَنفَقُواْ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡۚ فَٱلصَّٰلِحَٰتُ قَٰنِتَٰتٌ حَٰفِظَٰتٞ لِّلۡغَيۡبِ بِمَا حَفِظَ ٱللَّهُۚ وَٱلَّٰتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَٱهۡجُرُوهُنَّ فِي ٱلۡمَضَاجِعِ وَٱضۡرِبُوهُنَّۖ فَإِنۡ أَطَعۡنَكُمۡ فَلَا تَبۡغُواْ عَلَيۡهِنَّ سَبِيلًاۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيّٗا كَبِيرٗا ﴾
[النِّسَاء: 34]

Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الرجال قوامون على النساء بما فضل الله بعضهم على بعض وبما أنفقوا, باللغة السواحيلية

﴿الرجال قوامون على النساء بما فضل الله بعضهم على بعض وبما أنفقوا﴾ [النِّسَاء: 34]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wanaume ni wasimamizi wa kuwaelekeza wanawake na kuwatunza, kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu Amewatunuku nacho cha sifa za usimamizi na kutukuzwa, na mahari na matumizi waliyowapa hao wanawake. Basi wale walio wema katika wao, hao wanawake, kwa kuhifadhiwa na Mwenyezi Mungu na kuafikiwa, wanasimama imara kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu, wanamtii Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na wanatunza kila lisilojulikana na waume zao katika mambo waliyoaminiwa nayo. Na wale katika wao mnaochelea kuwafanyia nyinyi ujeuri kwa kuacha kuwatii, wapeni nasaha kwa maneno mazuri; iwapo maneno mazuri hayakuzaa matunda kwao, wahameni vitandani wala msiwakaribie. Iwapo kuwahama hakukuwafanya waathirike na kubadili mwenendo wao, basi wapigeni kipigo kisicho na madhara. Na wakiwa watawatii, jihadharini kuwafanyia maonevu. Kwani Mwenye zi Mungu Aliye juu, Aliye Mkubwa Ndiye Msaidizi wao, na Yeye ni Mwenye kuwalipiza wale waliowadhulumu na kuwaonea
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek