×

Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi 4:6 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:6) ayat 6 in Swahili

4:6 Surah An-Nisa’ ayat 6 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 6 - النِّسَاء - Page - Juz 4

﴿وَٱبۡتَلُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰ حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغُواْ ٱلنِّكَاحَ فَإِنۡ ءَانَسۡتُم مِّنۡهُمۡ رُشۡدٗا فَٱدۡفَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَأۡكُلُوهَآ إِسۡرَافٗا وَبِدَارًا أَن يَكۡبَرُواْۚ وَمَن كَانَ غَنِيّٗا فَلۡيَسۡتَعۡفِفۡۖ وَمَن كَانَ فَقِيرٗا فَلۡيَأۡكُلۡ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ فَإِذَا دَفَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ أَمۡوَٰلَهُمۡ فَأَشۡهِدُواْ عَلَيۡهِمۡۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبٗا ﴾
[النِّسَاء: 6]

Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliye kuwa tajiri naajizuilie, na aliye fakiri basi naale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao washuhudizieni. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وابتلوا اليتامى حتى إذا بلغوا النكاح فإن آنستم منهم رشدا فادفعوا إليهم, باللغة السواحيلية

﴿وابتلوا اليتامى حتى إذا بلغوا النكاح فإن آنستم منهم رشدا فادفعوا إليهم﴾ [النِّسَاء: 6]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wajaribuni mayatima walio chini ya mikono yenu mpate kuujua uwezo wao wa kutumia vizuri mali zao. Mpaka watakapofika miaka ya kubaleghe, mkawajua kuwa ni wema katika dini yao na wana uwezo wa kuhifadhi mali zao, basi wapeni mali zao. Wala msizifuje kwa kuzitumia mahali ambapo si pake kwa kupita mpaka wa matumizi na kukimbilia kuzila kabla hawajazichukua kutoka kwenu. Na mwenye mali katika nyinyi, ajizuie na atosheke na utajiri alionao, na asichukue chochote katika mali ya yatima. Na ambaye ni fukara, basi achukue kadiri ya haja yake wakati wa dharura. Na mtakapojua kuwa wao wana uwezo wa kuzihifadhi mali zao baada ya kubaleghe kwao na mkawapa mali zao, wawekeni mashahidi wakiwa ni dhamana kuwa mali yao yamewafikia kikamilifu, ili wasipate kulikanusha hilo. Na yawatosha nyinyi kwamba Mwenyezi Mungu ni shahidi juu yenu na Atawahesabu kwa mliyoyafanya
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek