Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 69 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّٰلِحِينَۚ وَحَسُنَ أُوْلَٰٓئِكَ رَفِيقٗا ﴾
[النِّسَاء: 69]
﴿ومن يطع الله والرسول فأولئك مع الذين أنعم الله عليهم من النبيين﴾ [النِّسَاء: 69]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mwenye kukubali amri za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na uongofu wa Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, basi hao ni wale ambao wana utukufu wa mambo na vyeo. Wao watakuwa pamoja na wale waliopewa neema na Mwenyezi Mungu miongoni mwa Mitume na wakweli wa Imani, ambao kuamini kwao yaliyoletwa na Mitume kulikamilika kiitikadi, kimaneno na kivitendo na mashahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na Waumini wema. Na wazuri wa marafiki wa mtu kuwa nao Peponi ni hao |