×

Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu. 4:78 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:78) ayat 78 in Swahili

4:78 Surah An-Nisa’ ayat 78 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 78 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿أَيۡنَمَا تَكُونُواْ يُدۡرِككُّمُ ٱلۡمَوۡتُ وَلَوۡ كُنتُمۡ فِي بُرُوجٖ مُّشَيَّدَةٖۗ وَإِن تُصِبۡهُمۡ حَسَنَةٞ يَقُولُواْ هَٰذِهِۦ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةٞ يَقُولُواْ هَٰذِهِۦ مِنۡ عِندِكَۚ قُلۡ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ فَمَالِ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلۡقَوۡمِ لَا يَكَادُونَ يَفۡقَهُونَ حَدِيثٗا ﴾
[النِّسَاء: 78]

Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu. Na likiwafikilia jema wanasema: Hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu. Na likiwafikilia ovu wanasema: Hili limetoka kwako wewe. Sema: Yote yanatokana na Mwenyezi Mungu. Basi wana nini watu hawa hata hawakaribii kufahamu maneno

❮ Previous Next ❯

ترجمة: أينما تكونوا يدرككم الموت ولو كنتم في بروج مشيدة وإن تصبهم حسنة, باللغة السواحيلية

﴿أينما تكونوا يدرككم الموت ولو كنتم في بروج مشيدة وإن تصبهم حسنة﴾ [النِّسَاء: 78]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Popote mliopo mtafikiwa na kifo, pawe ni mahali popote pale mnapokuwa, muda wenu ukikoma, hata kama mupo ndani ya ngome zilizoimarishwa zilizoko mbali na kiwanja cha mapambano na mapigano. Na wakipatikana na mambo ya kuwafurahisha ya starehe ya maisha haya (ya ulimwenguni), wanayanasibisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kuwa Ndiye Aliyewapatia, na watokewapo na matukio wanayoyachukia, wanayanasibisha kwa Mtume Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuwa yamesababishwa na yeye kwa ujinga wao na kwa fikira zao kuwa yeye amewaletea nuhusi. Na hawakujua kwamba yote yanatokana na Mwenyezi Mungu Peke Yake, kwa uamuzi Wake na makadirio Yake. Basi kwa nini wao hawakaribii kuelewa maneno yoyote unayowaelezea
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek