×

Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao 4:83 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:83) ayat 83 in Swahili

4:83 Surah An-Nisa’ ayat 83 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 83 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿وَإِذَا جَآءَهُمۡ أَمۡرٞ مِّنَ ٱلۡأَمۡنِ أَوِ ٱلۡخَوۡفِ أَذَاعُواْ بِهِۦۖ وَلَوۡ رَدُّوهُ إِلَى ٱلرَّسُولِ وَإِلَىٰٓ أُوْلِي ٱلۡأَمۡرِ مِنۡهُمۡ لَعَلِمَهُ ٱلَّذِينَ يَسۡتَنۢبِطُونَهُۥ مِنۡهُمۡۗ وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ لَٱتَّبَعۡتُمُ ٱلشَّيۡطَٰنَ إِلَّا قَلِيلٗا ﴾
[النِّسَاء: 83]

Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وإذا جاءهم أمر من الأمن أو الخوف أذاعوا به ولو ردوه إلى, باللغة السواحيلية

﴿وإذا جاءهم أمر من الأمن أو الخوف أذاعوا به ولو ردوه إلى﴾ [النِّسَاء: 83]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na likiwajia, hawa ambao Imani haijakita ndani ya nyoyo zao, jambo ambalo inapasa lifichwe linalofungamana na usalama, ambao heri yake itarudi kwa Uislamu na Waislamu, au hofu, ambayo inatia babaiko ndani ya nyoyo zao, wanalitoa nje na kulitangaza kwa watu. Na lau wao walilipeleka, lile liliowajia, kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye na kwa wenye ujuzi na ufahamu, wangaliujua uhakika wake wale wachambuzi kati yao. Na lau si Mwenyezi Mungu kuwafanyia wema na kuwaonea huruma, Mungalimfuata Shetani na mawazo mnayotiwa naye, isipokuwa wachache katika nyinyi
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek