Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 25 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡحَقِّ مِنۡ عِندِنَا قَالُواْ ٱقۡتُلُوٓاْ أَبۡنَآءَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ وَٱسۡتَحۡيُواْ نِسَآءَهُمۡۚ وَمَا كَيۡدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ ﴾
[غَافِر: 25]
﴿فلما جاءهم بالحق من عندنا قالوا اقتلوا أبناء الذين آمنوا معه واستحيوا﴾ [غَافِر: 25]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi Mūsā alipomjia Fir'awn, Hāmān na Qārūn kwa miujiza iliyo waziwazi kutoka kwetu, hawakutosheka kwa kuipinga na kuikanusha , bali walisema, «waueni wana wa kiume wa wale walioamini pamoja naye na waacheni wanawake wao watumike na wafanywe watumwa. Na haikuwa mipango ya makafiri isipokuwa ni yenye kupita na kuangamia |